Wednesday, November 2, 2016

UGANDA: RAISI YOWERI MUSEVENI ATOA AMRI YA KUFUNGWA KWA CHUO KIKUU CHA MAKERERE


Chuo kikuu cha Makerere ni kimoja kati ya vyuo vikuu vikongwe Afrika. siku ya juma nne jana tarehe 1/novemba ndipo raisi wa Uganda alipo toa amri ya kufungwa kwa chuo kikuu hicho, kufuatia maandamano ambayo yalikuwa yanaendeshwa na waalimu pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu hicho cha makerere.

Walimu wa chuo hicho ndio walio anzisha maandamano wakidai kuto ongezwa kwa mishahara yao kama walivyo kuwa wame ahidiwa, pia yapata miezi minane sasa hawajapata mishahara yao na kuidai serikari kuwalipa.

walimu hao walichukua hatua ya kugoma kufundisha na kufanya maandamano, na wanafunzi kuto kukubaliana na kitendo cha walimu wao na wao pia kufanya maandamano.

siku ya jana raisi Yoweri Museveni wa Uganda ndipo alipo chukua uamuzi wa kufunga chuo hicho kikuu cha Uganda (Makerer).

Sababu kubwa ya kufungwa kwa chuo hiki ni kuepukana na hasara ambayo husababishwa na uharibifu wa vifaa vya shule kipindi cha maandamano.

No comments:

Post a Comment