Friday, April 29, 2016

KITOKO BIBARWA MSANII TOKA RWANDA ANAKUJA NA ALBUM YA POLE POLE

Kitoko ni msanii wa Rwanda aishiye inchini Wingereza ametakngaza kuacia album yake yenye videos tano ambayo ameipa jina la Pole Pole.


Baada ya msanii Kitoko kuachia video yake mpya "Am In Love" ambayo alifanya na muimbaji wa kike maarufu Sheebah Kalungi kutoka nchini Uganda.


Sasa anaendelea kushtua watu kwa kutangaza kuja na album mpya ya videos yenye nyimbo tano ambazo ni 1- Hatuwezi Kurudi 2- Ninde 3- Pole Pole 4- Biragoye 5- Amadayimoni. Ametangaza kuwa baada ya week mbili zijazo album itakuwa imetoka



Monday, April 25, 2016

NEW VIDEO : NAVIO - NJOGEREZA (OFFICIAL VIDEO 2016)



Msanii wa Hip Hop toka pande za Uganda Navio ambae alikuwa kwenye kundi la mziki wa Hip hop Clear Cut na baadae kufanya mziki kama solo artist na kuendelea ku upeleka mbali mziki wake sasa ka achia video mpya itwayo Njogereza

PAPA WEMBA MUIMBAJI WA CONGO ALIANGUKA AKIWA JUKWAANI NA KUFARIKI DUNIA

Muimbaji Maarufu toka Congo Papa Wemba afariki Dunia akiwa na Miaka 66 aki anguka jukwaani akiwa anaimba, 



Video zinaonyesha akianguka jukwaani nyuma ya wachezaji mziki wake kabla ya kupata huduma ya kwanza

Mwana Muziki huyo alijijengea umaarufu mkubwa kwa miondoko yake yaki Afrika  huku aki changanya na miondoko yaki Cuban na kufanya mziki wake kuwa mziki waki pekee na maarufu sana duniani.

Mwana Mziki huyu aliwahi kuzunguka nchi nyingi sana duniani akifanya matamasha mbalimbali, aliwahi pia kufanya nyimbo na mwanamziki maarufu wa wingereza  Peter Gabriel. Papa wemba kafanya mengi katika mziki wa Congio na Africa kwa ujumla wqwatu wengi wamejalibu kumfananisha na msanii Fela Kuti kwa ustadi wa mziki Africa. 

Papa Wemba alianza kujiskia ni mgonjwa siku ya Jumamosi asubuhi na baadaye kuiaga dunia akiwa jukwaani ila sababu za kifo chake mpaka sasa hazijulikani

Alifariki wakiwa bado hawajamfikisha Hospitalini kwa taarifa zilizo tolewa na msemaji wa police wa Ivosep Morgue huko Abjdan 

Mwanamziki huyu alizaliwa mwaka 1949 majina yake ya kuzaliwa yakiwa ni Shungu Wembadio Pene Kikumba aliaza kugundua kipaji chake cha kuimba ikiwa kama muimba kwaya wa kanisani.

Papa Wemba ni msanii aliye saidia sana kukuza mziki wa Congo wa miondoko ya Rhumba kwa style zake za Soukous ambazo zimekuja kuwa ni maarufu sana nchini Africa. 

Pamoja na band yake ya mziki ya Zaiko Langa Langa, Isifi na Viva la Musica wameweza kufanya hits nyingi ikiwemo L'Escrave na le Voyageur.




NEW VIDEO : KNOWLESS BUTERA - KO NASHIZE (OFFICIAL VIDEO 2016)


Artist: Knowless Butera

Mwanadada mrembo na muimbaji wa Rwanda Butera Knowless katoa video yake mpya inayo itwa Ko Nashize, video imefanywa na video director Iba Lab ni director wa videos ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu ila sasa karudi na kasi. Hapa chini unaweza kuangalia hiyo video



Friday, April 22, 2016

MWANA MZIKI MKONGWE PRINCE ROGERS NELSON WA MAREKANI AFARIKI DUNIA

                                                       PRINCE ROGERS NELSON 

Msanii mashuhuri na mkongwe PRINCE ROGERS NELSON ambaye alikuwa Muimbaji, Muandishi, mchezaji wa vifaa mbali mbali vya muziki, Producer  na pia muigizaji amefariki dunia siku ya jana tarehe 21.04.2016. ali fariki akiwa kwenye lift na mpaka sasa bado haija julikana sababu ya kifo chake police ya Marekani bado inafuatilia sababu ya kifo chake.
Muimbaji huyu atakumbukwa sana na watu wengi duniani kwani alikuwa mkali wa miondoko ya Funk, Rocky, RnB, Soul pamoja na Pop.
Mwana mziki huyu alizaliwa Marekani huko Minneapolis Minnesota  June. 7. 1958 na kufariki dunia tarehe 21 April 2016. Mungu ailaze roho yake mahari pema.

Thursday, April 21, 2016

MSANII MAKO NIKOSHWA ATANGAZA KUWA NA AFYA NZURI SASA NA KURUDI STUDIO KUFANYA MZIKI

Msanii mkongwe wa miondoko ya Afro Beat pamoja na Dancehall nchini Rwanda Mako Nikoshwa alimaliza mda mrefu akiwa mgonjwa na kulazwa hospitali kwa mda sasa yuko na afya njema na tayali amerudi studio kuendelea na mziki. akiongea na UP IN KGL alituambia kuwa " Namshukuru Mungu kuni wezesha kupona  nilikuwa nimeugua kwa muda mrefu na sikuamini kama nitaweza kurudi kuwa na hali nzuru, ila sasa niko salama na afya nzuri, Na nimefurahi kuweza kurudi stuio kuendeleza mziki wangu na kuku tana na wasanii wenzangu.

                                          Mako Nikoshwa, Rafiki na Miss Confidence

Tarehe 16 mwezi wa 4 mwaka 2016 Camera zetu zilimpata Msanii Mako Nikoshwa akiwa Studio za T-Time Pro Maeneo ya Kimironko Mjini Kigali Rwanda akiwa pamoja na wenzake Rafiki Coga pamoja na mwanadada Miss Confidence wakiwa studio wana Record nyimbo mpya ambayo wame tutangazia kuwa ita itwa Ndi Umunyarwanda. walionekana  wakiwa na furaha kubwa kwanza kwa wasanii wenzake kama Miss Confidence pamoja na Rafiki wali shindwa kujizuia na kututangazia kuwa wana furaha kubwa kufanya nyimbo na Mako ambapo wengi hawakutegemea kama atarudi studio.

Hapa chini ni baadhi ya picha ambapo Makoni Koshwa akiwa na wasanii wenzake ndani ya studio kama  vile Rafiki Coga, Miss Confidance, Bac-t Blastmaster, Tru-D, Senge na Producer DJ-B





Wednesday, April 20, 2016

Msanii Rapper Chidi Benzi Wa Tanzania Adai Kuwa Sasa Yuko Sawa Baada Ya Kutimiza Mwezi ndani Ya Sobber House

“Sina mengi ya kuongea, niko sawa, nipo okay, niko fresh na msaada naupata,” anasema Chidi Benz kwenye video iliyowekwa kwenye Instagram na Kalapina.



Rapper huyo anatimiza mwezi tangu aingie sober house. Kuna mabadiliko makubwa katika muonekano wake ukilinganisha na jinsi alivyokuwa wakati akiingia. Afya yake ilikuwa imedhoofika kwa kiasi kikubwa na kuwatisha watu wengi hadi kumfanya Babutale amshauri aingie sober house.
“Ni safari ya Chidi Benz na harakati na hapa ni siku 27 ndani ya sober house mshkaji anaendelea vizuri sana kilichobaki ni kumuombea kwa mungu asiweze kurejea tena katika matumizi ya dawa za kulevya safari nzima ya chid benz utaiona kupitia kipindi cha harakati cloudstv stay tuned,” ameandika Kalapina.
Chidi Benz yupo Bagamoyo Sober House.