Monday, May 23, 2016

BAC-T ATANGAZA UJIO WAKE MPYA KI MUZIKI NA HARAKATI ZA KUIKAMATA AFRIKA MASHARIKI



Msanii toka pande za Rwanda Bac-t a.k.a Blastmaster katangaza ujio wake mpya ki muziki na kusema kuwa anataka kufanya kazi zaidi kama msanii wa Afrika mashariki8 zaidi ya kufanya kazi kama local artist.

Bac-t amesema kuwa kwa sasa anafanya mziki sio wa kupigwa kwenye media bila mpango ila ni mziki ambao anataka upigwe kwenye media houses ki mpango na uweze kufika mbali. kwani kwa mtazamo wake anaona kuwa mziki kuutoa bila video na kutegemea promo ya radio station pekee ni bule. kwa sasa ana mpango wa kufanya album yake ambayo ipo kwenye miondoko ya Dancehall, japokuwa watu wengi wamemzoea kufanya miondoko ya Hip Hop. Tulipo muuliza kwanini kaamua kufanya hivyo, aameseme kuwa anafanya mziki ki biashara zaidi ya mziki wa kujifurahisha ndio maana kaamua kufanya mziki wenye miondoko ya kucheza pia ndani yake awapatie wasikilizaji ujumbe husika.

                                                 Amore and Bac-t

Akiendelea kagusia njia anazoenda kutumia kupeleka mbali mziki wake, "Niko na mpango wa kufaya video nyingi sana ikiwemo video mpya ambayo nimefanya na Amore mwanadada muimbaji Mnyarwanda ambaye anaishi Europe kwa ajili ya Masomo, Video hii itatoka hivi karibuni kwani maandalizo yote ni kama yame kamilika inaitwa I STILL LOVE YOU.
Video hii imefanywa na Video Director ambaye kwa sasa anakuja kwa kasi kijana Nameless


Na baada ya hapo amesema kuwa ata dondosha album ambayo itakuwa na nyimbo 10 kabla mwishoni mwa mwaka huu.
Ame endelea kusema kuwa East Africa lazima imtambue kama msanii ambaye ana uwezo ki muziki na anataka kuiweka nchi yake kwenye ramani ya mziki mzuri duniani.

No comments:

Post a Comment