Follow by Email

Thursday, June 15, 2017

JOSE CHAMELEONE NA DANIELLA WAME ZUNGUMZIA JINSI WALIVYO TATUA UTATA ULIOTAKA KUSABABISHA WA TENGANE
Yapata mwezi mzima sasa tangu kusikia utata ndani ya nyumba ya  Joseph Mayanja [Jose Chameleone] kulizungumziwa mengi ikiwemo utata uliotaka kusababisha wawili hao kutengana, lakini wawili hao wameamua kumaliza utata na kurudi kuishi pamoja bila matatizo.

Chameleone na Daniella walifunga ndoa tarehe 7 mwezi wa 6 mwaka 2008 ndani ya kanisa la  Biina Catholic Church lililoko maeneo ya Mutungo huko nchini Uganda. Wakati wa harusi yao walifanya sherehe za hari ya juu hadi kusababisha vyombo vya habari kuzungumzia sana harusi yao, hadi sasa familia hii ina watoto wane ambao ni  Abba Marcus Mayanja, Alfa Joseph Mayanja, Alba Shyne Mayanja n’uwitwa Amma Mayanja.


Siku chache zilizo pita vyombo vya habari vili zungumza kuwa mke wa Chameleone alipeleka mashitaka mahakamani akidai kuachana na mmewe..  wakati huo Daniella aliandika kuwa uvumilivu umemshinda na hataki tena kuendelea kuishi na mmewe waliye maliza miaka zaidi ya 9 wakiwa pamoja. Akiomba mahakama kuwa tenganisha ili kila mmoja aendelee na maisha yake.. 

Katika mashitaka ya mama huyu alisema kama Jose Chameleone hata acha tabia mbaya zinazo sababishwa na utumiaji wa vilevi basi mahusiano yao yatakwisha kabisa.. na pia mama huyu alitangaza kuwa Chameleone amekuwa akimfanyia mambo mabaya mengi kuanzia mwaka wa 2013 hadi kufikia hatua ya kumtishia kumu uwa . baada ya mwezi mzima wa habari ambazo hazikuwa nzuri kwa mashabiki wa Chameleone sasa ana onekana kuwa yuko vizuri na mkewe. Kwenye interview ya  Chameleone na Daniella waliyo ifanya na gazeti la The New Vision, wamesema kuwa hivi sasa wame tatua tofauti zao na mashitaka yaliyo kuwa yametolewa na Daniella tayali yamefutwa huko mahakamani..
No comments:

Post a Comment