Raisi Kagame ameonyesha kuwa kufanya kazi pamoja kama jumuia ya nchi za Afrika Mashariki itasababisha nchi zote kuwa na nguvu kuliko kila nchi kujitegemea.
Alisema kuwa "Kwanza kabisa tunapaswa kuweka bidii na kujituma katika mitazamo na mipango tuliyo jiwekea kama jumuia, na pia kuweka bidii katika utendaji wa kazi nzuri na zenye manufaa.
Huu muungano una tusababishia kuwa na nguvu kuliko pale ambapo kila nchi ikijitegemea. lakini hapa tunapaswa muda wote kuwa pamoja na kushirikiana ili tuweze kutekeleza yale yote tunayo kubaliana".
Raisi John Pombe Magufuli wa Tanzania, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda na makamu wa raisi wa Kenya William Ruto. Hawa ndio viongozi waliokutana.
Sudani ya mashariki ili wakilishwa kama nchi ya sita ambayo nayo ikiwemo katika jumuia ya nchi za Afrika Mashariki japo kuwa raisi wa nchi hiyo Salva Kiir hakuwepo kwenye mkutano huo.
Pia maswala ya Burundi yali zungumziwa katika mkutano huo, raisi Pierre Nkurunziza hakuwepo lakini ali wakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje bwana Alain Aime Nyamitwe.
Msuruhishi wa maswala ya Burundi bwana Benjamini William Mkapa aliwakilisha faili ambalo lina eleza pale mambo yalipo fika katika jukumu la kutafuta amani nchini Burundi.
Kiongozi wa EAC raisi John Pombe Magufuli alimshukuru bwana Benjamini Mkapa kwa kazi ambayo ana ifanya kama mkutanishi katika maswala ya kutafuta amani ya Burundi.
No comments:
Post a Comment