Wednesday, April 20, 2016

Msanii Rapper Chidi Benzi Wa Tanzania Adai Kuwa Sasa Yuko Sawa Baada Ya Kutimiza Mwezi ndani Ya Sobber House

“Sina mengi ya kuongea, niko sawa, nipo okay, niko fresh na msaada naupata,” anasema Chidi Benz kwenye video iliyowekwa kwenye Instagram na Kalapina.



Rapper huyo anatimiza mwezi tangu aingie sober house. Kuna mabadiliko makubwa katika muonekano wake ukilinganisha na jinsi alivyokuwa wakati akiingia. Afya yake ilikuwa imedhoofika kwa kiasi kikubwa na kuwatisha watu wengi hadi kumfanya Babutale amshauri aingie sober house.
“Ni safari ya Chidi Benz na harakati na hapa ni siku 27 ndani ya sober house mshkaji anaendelea vizuri sana kilichobaki ni kumuombea kwa mungu asiweze kurejea tena katika matumizi ya dawa za kulevya safari nzima ya chid benz utaiona kupitia kipindi cha harakati cloudstv stay tuned,” ameandika Kalapina.
Chidi Benz yupo Bagamoyo Sober House.

No comments:

Post a Comment