Mwanamuziki maarufu King
Kaka amechaguliwa kuwa balozi wa shirika la umoja wa mataifa la huduma kwa
watoto,UNICEF -Kaka alitangaza habari hiyo njema kwenye mtandao wake wa kijamii
wa Instagram Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za aina ya Rap,Kaka King Ametupia
ujumbe kwenye mtandao wake wa instagram
siku ya jumatano.mwanamuziki
huyo alizindua nyimbo mpya inayoitwa ’Yap Yap’. Bila kuchelewa siku iliyofuata
King aka dondosha ngoma nyingine mpya na
kupa jina ‘Life na adabu’. Kando na hayo
mwanamuziki huyo amechaguliwa kuwa balozi wa shirika la umoja wa mataifa la
huduma kwa watoto, UNICEF. Akionyesha furaha yake kwenye ujumbe aliouchapicha
kwenye ukurasa wake wa Instagram, King alisema kufanikiwa kwake kunatokana na
bidii.
“ Ungana nami ninaposhirikiana na shirika la
Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kujadili jinsi ya kuishi maisha
bila tashwishwi,”King aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. King
anajulikana kwa miziki zake zilizovuma kama,Niko kwa jam nakam Dodoma. Swahili shakespere
nazingine nyingi.
No comments:
Post a Comment