Thursday, June 15, 2017

MSANII RAPER WA KIKE WA NCHINI RWANDA CINEY KUFANYIWA BRIDAL SHOWER



Rapa Uwimana Aïsha maarufu kama [Ciney] pamoja na  Tumusiime Ronald mapenzi yao yamefika mbali baada ya kupendana kwa muda mrefu
Ciney na Tumusiime Ronald wamekula kiapoa cha kuishi pamoja kama mke na mume ki sheria za nchini Rwanda ambazo zina wahusu wanaotaka kufunga ndoa, kiapo hiki kimefanyikia Kimihurura tarehe  ya 12 mwezi wa tano 2017.



Ni mwezi mzima sasa baada ya wawili hawa kuapiswa ki sheria, na sasa msanii huyu kafanyiwa sherehe za Kitchen Part maarufu kama Bridal Shower, sherehe hizo zili hudhuriwa na rafiki zake wa karibu, wasichana na wanawake marafiki wa, watu hao wote wameonekana kumpa zawadi nyingi..

Sherehe za Bridal Shower ya Ciney zimefanyikia mjini  Kigali karibu na hospitali ya CHUK siku ya juma pili ya tarehe  11 mwezi wa 6 2017. Katika sherehe hizo ameonekana msanii wa kike maarufu wa nyimbo za injiri Tonzi aki imba..

Msanii huyu atafunga ndoa rasmi mwezi wa 7 / 2017,  inatangazwa kuwa atafungia ndoa ndani ya kanisa la wa Angilikana St Etienne Nyamirambo, na siku chache zilizo pita kanisa hilo lilimpokea rasmi kama muumini wake.
Ciney pamoja na mpenzi wake  Ronald wamekuwa pamoja kama wapenzi kwa muda wa  miaka minne sasa. Ronald alimvalisha pete ya uchumba Ciney kwenye tamasha la Comedy huko Serena Hotel tarehe 26 mwezi wa tatu 2017.













No comments:

Post a Comment