Monday, May 30, 2016

SALAX AWARDS IMERUDI TENA NA CATEGORIES 15 ZA WATAKAO WANIA TUZO HIZO.

Baada ya kuwa mashindano haya ya tuzo za Salax Awards za nchini Rwanda kuwa zime simama kwa muda mrefu sasa tuzo hizi zimerudi tena na kutangaza vipengele 15 vya watakao wania tuzo hizo. Kwa mujibu wa waandaji ambao ni Ikirezi Group na Yes Africa ltd.



Mashindano haya yanarudi tena kwa mara ya 6 sasa na vipengere 15 vya wawaniaji. ambapo sasa mashabiki wanajiuliza je itakuwa sawa wakati huu ama bado Mashindano haya yatabaki kuwa na dosari kama ilivyokuwa hapo awali .

Tazama hapa chini vipengele vyote vilivyomo ndani ya tuzo hizi.


CHRISS BROWN AMTAJA WIZ KID KUWA NAE KATIKA ONE HELL OF A NIGHT TOUR HUKO ULAYA

Msanii kutoka Nigeria Wiz Kid kwa sasa anaishi ile ndoto ambayo wasanii wengi wa Africa bado wanaiota.Baada ya kushilikishwa na Drake kwenye wimbo wake wa One Night Dance, wimbo uliomo kwenye album mpya ya Drake na ulishika number moja kwenye chart za billboard top 100. Nasasa msanii kutoka pande za Nigeria Wiz Kid kupata bonge la shavu kumsindikiza Drake kwenye Tour ambazo anafanya kwa sasa Ulaya "One Hell Of A Night Tour.

Taarifa hiyo ilitolewa na Chris Brown mwenyewe kwenye akaunti yake ya Instagram kabla ya Wizkid naye kuandika: 5th – 11th June I’ll be supporting my brother @chrisbrownofficial !! Get ur tickets!! #Onehellofanitetour Bringing the African wave!!”

Wizkid ana wimbo aliomshirikisha muimbaji huyo wa Marekani mwenye mashabiki wengi.

Friday, May 27, 2016

JOSE MOURINHO ATANGAZWA RASMI KUWA MANAGER MPYA WA MANCHESTER UNITED

Klabu ya Manchester United leo imemtangaza rasmi Mreno Jose mourinho kuwa manager mpya wa klabu hiyo. Ali kabidhiwa uongozi huo ukitoka mikononi mwa mholanzi Louis Van Gaal aliye timuliwa kutoka timu hiyo ivi karibuni.


Mourinho mwenye umri wa miaka 54 ambaye aliwahi kuvifundisha vilabu vya Porto, Chelsea, Inter Milan pamoja na Real Madri. Ame saini mkataba wa miaka miitatu kuwatumikia mashehani hao wekundu.
"Kuwa Manager wa Manchester United ni heshima  kubwa sana. Ni klabu inayo fahamika na kupendwa na watu wengi duniani kote" amesema Jose.

Mreno huyo ambaye ni mzoefu a kushida mataji ata anza rasmi kutumikia klabu hiyo kuanzia msimu wa 2016/2017.

Tuesday, May 24, 2016

KAMA GIRLFRIEND WAKO HAFANYI MAMBO HAYA, KUNA TATIZO


1. Ni shabiki wako namba moja, siku zote
Kama haungi mkono kila hatua unayopiga kwenye maisha yako na yote unayotaka kufanya ni muda wa kufikiria upya uhusiano huo. Haijalishi ni kitu gani unafanya, ni muhimu awe nyuma yako kukupa support.
2. Anakupa muda wa kupumua
Kuna tofauti kati ya kujali na kuwa kupe. Ni kawaida kwake kukuangalia hapa na pale kujua siku yako inaendaje, lakini kama anatokea tu hovyo kazini kwako kila siku, hiyo inaweza kuwa ni issue.
3. Anakubali marafiki zako – ama walau anajifanya kuwajali
Kama hawapendi marafiki zako, hakuna jinsi utaweza kuchagua kati yao na yeye. Kama anakulazimisha kuchagua kati ya pande hizi mbili basi ni muda wa kumwacha aende. Kama anakupenda kweli hatakufanya uchague kati yao na yeye.

4. Anaipenda familia yako kama unavyoipenda
Hili ni muhimu. Kama haelewani na ndugu zako ni ngumu sana kudumu naye. Kama familia yako ni muhimu zaidi kwako atapenda kuwa karibu nao kama unavyopenda. Kama huleta ugomvi kila mnapoenda kwa wazazi wako ama anapokupa visingizio vya kutoenda, basi hakufai.
5. Yuko tayari kwa lolote, ilimradi yuko nawe
Hii ina maana kuwa anakuwa tayari na ameridhika kuwa nawe. Kama kila siku analalamika juu ya vyote unavyotaka kufanya huenda hamko kwenye ukurasa mmoja.
6. Anakupenda kama ulivyo
Kama mara zote huudhiwa na vitu kuhusu kadhaa kuhusu wewe, huenda akawa anataka kukubadilisha na sio kukupenda kama ulivyo. Kama huna uhakika kuwa anakupenda ulivyo, basi ni muda wa kusonga mbele.

Monday, May 23, 2016

VIDEO: ADELE – ‘SEND MY LOVE (TO YOUR NEW LOVER)’


Fresh off her win for Top Billboard 200 Album at the Billboard Music Awards, Adele debuted the video for her new single “Send My Love (To Your New Lover)” during Sunday’s live broadcast. Donning a floral dress, the British songstress keeps it simple in the Patrick Daughters-directed clip, using layered effects of herself spinning and dancing.
The Max Martin-produced song is the third single off her chart-topping album 25. On July 5, she will launch her North American tour at Xcel Energy Center in St. Paul, Minn.
Watch Adele get trippy below.

BAC-T ATANGAZA UJIO WAKE MPYA KI MUZIKI NA HARAKATI ZA KUIKAMATA AFRIKA MASHARIKI



Msanii toka pande za Rwanda Bac-t a.k.a Blastmaster katangaza ujio wake mpya ki muziki na kusema kuwa anataka kufanya kazi zaidi kama msanii wa Afrika mashariki8 zaidi ya kufanya kazi kama local artist.

Bac-t amesema kuwa kwa sasa anafanya mziki sio wa kupigwa kwenye media bila mpango ila ni mziki ambao anataka upigwe kwenye media houses ki mpango na uweze kufika mbali. kwani kwa mtazamo wake anaona kuwa mziki kuutoa bila video na kutegemea promo ya radio station pekee ni bule. kwa sasa ana mpango wa kufanya album yake ambayo ipo kwenye miondoko ya Dancehall, japokuwa watu wengi wamemzoea kufanya miondoko ya Hip Hop. Tulipo muuliza kwanini kaamua kufanya hivyo, aameseme kuwa anafanya mziki ki biashara zaidi ya mziki wa kujifurahisha ndio maana kaamua kufanya mziki wenye miondoko ya kucheza pia ndani yake awapatie wasikilizaji ujumbe husika.

                                                 Amore and Bac-t

Akiendelea kagusia njia anazoenda kutumia kupeleka mbali mziki wake, "Niko na mpango wa kufaya video nyingi sana ikiwemo video mpya ambayo nimefanya na Amore mwanadada muimbaji Mnyarwanda ambaye anaishi Europe kwa ajili ya Masomo, Video hii itatoka hivi karibuni kwani maandalizo yote ni kama yame kamilika inaitwa I STILL LOVE YOU.
Video hii imefanywa na Video Director ambaye kwa sasa anakuja kwa kasi kijana Nameless


Na baada ya hapo amesema kuwa ata dondosha album ambayo itakuwa na nyimbo 10 kabla mwishoni mwa mwaka huu.
Ame endelea kusema kuwa East Africa lazima imtambue kama msanii ambaye ana uwezo ki muziki na anataka kuiweka nchi yake kwenye ramani ya mziki mzuri duniani.

Friday, May 20, 2016

PREZZO KUMVALISHA PETE YA UCHUMBA BINTI MICHELLE OYOLA


Rapper kutoka Kenya Prezzo ame mvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Michelle Oyola ambaye hivi kalibuni wamekuwa pamoja sana sehemu mbali mbali ambapo Prezzo alipo onekana.

Prezzo aliwahi kufanya mambo sawa sawa na haya kwa wanawake wawili tofauti akiwemo mama watoto wake Daisy na maremu Goldie, Kwa sasa mitandao ya kijamii nchini Kenya imepata taarifa hizi ni kuongelea kwa sana kuwa huyu bint wakati huu ni lazima atakuwa mke wa Prezzo.


DIAMOND PLUTNUMZ ATAJWA KUWANIA TUZO ZA BET AWARDS 2016

Msanii Diamond kutoka Tanzania atajwa kuwania tuzo za BET awards za mwaka huu wa 2016 ikiwa ni mara yake ya pili akiwa katika tuzo hizo, akiwa katika kipengele cha Best International Act Africa

Katika Awards hizo Diamonds Plutnumz atakuwa akichuana na wengine kama Wizkid, Yemi Olade, AKA, Casper Nyovest, MZVEE, Serge Beynaud na Black  Koffie wa Afrika Kusini


Tuzo hizo zita tolewa mwishoni mwa mwezi June Nchini Marekani na msanii huyu atakuwa aki perfom June 26 huko nchini Marekani.