Msanii mkongwe wa miondoko ya Afro Beat pamoja na Dancehall nchini Rwanda Mako Nikoshwa alimaliza mda mrefu akiwa mgonjwa na kulazwa hospitali kwa mda sasa yuko na afya njema na tayali amerudi studio kuendelea na mziki. akiongea na UP IN KGL alituambia kuwa " Namshukuru Mungu kuni wezesha kupona nilikuwa nimeugua kwa muda mrefu na sikuamini kama nitaweza kurudi kuwa na hali nzuru, ila sasa niko salama na afya nzuri, Na nimefurahi kuweza kurudi stuio kuendeleza mziki wangu na kuku tana na wasanii wenzangu.
Mako Nikoshwa, Rafiki na Miss Confidence
Tarehe 16 mwezi wa 4 mwaka 2016 Camera zetu zilimpata Msanii Mako Nikoshwa akiwa Studio za T-Time Pro Maeneo ya Kimironko Mjini Kigali Rwanda akiwa pamoja na wenzake Rafiki Coga pamoja na mwanadada Miss Confidence wakiwa studio wana Record nyimbo mpya ambayo wame tutangazia kuwa ita itwa Ndi Umunyarwanda. walionekana wakiwa na furaha kubwa kwanza kwa wasanii wenzake kama Miss Confidence pamoja na Rafiki wali shindwa kujizuia na kututangazia kuwa wana furaha kubwa kufanya nyimbo na Mako ambapo wengi hawakutegemea kama atarudi studio.
Hapa chini ni baadhi ya picha ambapo Makoni Koshwa akiwa na wasanii wenzake ndani ya studio kama vile Rafiki Coga, Miss Confidance, Bac-t Blastmaster, Tru-D, Senge na Producer DJ-B
No comments:
Post a Comment