Thursday, June 15, 2017

Aliyeonekana akimshika Zari anena



Mwanaume ambaye aliyedaiwa kumshika mzazi mwenza wa msanii Diamond Plutnumz, Zari Hassani katika bwawa la kuogelea, Edwin Lutaaya amefunguka juu ya tuhuma hizo.
Edwin ambaye ni ndugu wa mume wa zamani wa Zari, amedai kuwa hakumshika Zari kama mitandao ilivyodai na ile picha ilipigwa na mkewe ambaye naye alikuwepo katika eneo hilo.
Edwin ambaye amefanya mahojiano kwa njia ya simu na Kakensa Media, amesema kuwa “This goes out to Diamond, I know you can’t hear much of Luganda… I never meant to offend you neither did I touch Zari’s bums, you misquoted the whole situation. That picture was taken with decency, we never even took any closure next to each other.
“Deep down in my heart I don’t have any intentions of hitting or proposing to my in-law (Zari), in our custom it doesn’t allow that. And I want to make it very clear this this moment… please I respect your family and I respect your relationship with Zari. I can never come in between us or anyone in our family, I will never come between you. ” alionge Edwin

VANNESA MDEE NA NAVIO WAKUTANA NA KUFANYA VIDEO PAMOJA HUKO NCHINI UGANDA



Ulijua baada ya kukutana kwa Vanessa Mdee wa Tanzania  na Navio kutoka Uganda ndio imeishai pale? Basi kaa tayari kwa wimbo mpya kutoka kwa wasanii hao.


Wawili hao wameonekana tayari kuna kitu wameshakiandaa kwa ajili ya mashabiki wao kutokana na baadhi ya picha walizoziweka kwenye mitandao yao ya kijamii.
Vanessa ambaye wiki iliyopita alionekana akiwa nchini Uganda na kukutana na rapper huyo, ameweka picha kadhaa kwenye mtandao wake wa Instagram zikiwaonyesha wakiwa location wakishoot video ya wimbo wao huo.
Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha wawili hao wakiwa wanashoot video hiyo.






MWANAMZIKI KING KAKA WA KENYA APEWA KAZI NA UMOJA WA MATAIFA




Mwanamuziki maarufu King Kaka amechaguliwa kuwa balozi wa shirika la umoja wa mataifa la huduma kwa watoto,UNICEF -Kaka alitangaza habari hiyo njema kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za aina ya Rap,Kaka King Ametupia ujumbe kwenye mtandao wake wa instagram

siku ya jumatano.mwanamuziki huyo alizindua nyimbo mpya inayoitwa ’Yap Yap’. Bila kuchelewa siku iliyofuata King aka dondosha  ngoma nyingine mpya na kupa jina  ‘Life na adabu’. Kando na hayo mwanamuziki huyo amechaguliwa kuwa balozi wa shirika la umoja wa mataifa la huduma kwa watoto, UNICEF. Akionyesha furaha yake kwenye ujumbe aliouchapicha kwenye ukurasa wake wa Instagram, King alisema kufanikiwa kwake kunatokana na bidii.
 “ Ungana nami ninaposhirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kujadili jinsi ya kuishi maisha bila tashwishwi,”King aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. King anajulikana kwa miziki zake zilizovuma kama,Niko kwa jam nakam Dodoma. Swahili shakespere nazingine nyingi.

JOSE CHAMELEONE NA DANIELLA WAME ZUNGUMZIA JINSI WALIVYO TATUA UTATA ULIOTAKA KUSABABISHA WA TENGANE




Yapata mwezi mzima sasa tangu kusikia utata ndani ya nyumba ya  Joseph Mayanja [Jose Chameleone] kulizungumziwa mengi ikiwemo utata uliotaka kusababisha wawili hao kutengana, lakini wawili hao wameamua kumaliza utata na kurudi kuishi pamoja bila matatizo.

Chameleone na Daniella walifunga ndoa tarehe 7 mwezi wa 6 mwaka 2008 ndani ya kanisa la  Biina Catholic Church lililoko maeneo ya Mutungo huko nchini Uganda. Wakati wa harusi yao walifanya sherehe za hari ya juu hadi kusababisha vyombo vya habari kuzungumzia sana harusi yao, hadi sasa familia hii ina watoto wane ambao ni  Abba Marcus Mayanja, Alfa Joseph Mayanja, Alba Shyne Mayanja n’uwitwa Amma Mayanja.


Siku chache zilizo pita vyombo vya habari vili zungumza kuwa mke wa Chameleone alipeleka mashitaka mahakamani akidai kuachana na mmewe..  wakati huo Daniella aliandika kuwa uvumilivu umemshinda na hataki tena kuendelea kuishi na mmewe waliye maliza miaka zaidi ya 9 wakiwa pamoja. Akiomba mahakama kuwa tenganisha ili kila mmoja aendelee na maisha yake.. 

Katika mashitaka ya mama huyu alisema kama Jose Chameleone hata acha tabia mbaya zinazo sababishwa na utumiaji wa vilevi basi mahusiano yao yatakwisha kabisa.. na pia mama huyu alitangaza kuwa Chameleone amekuwa akimfanyia mambo mabaya mengi kuanzia mwaka wa 2013 hadi kufikia hatua ya kumtishia kumu uwa . baada ya mwezi mzima wa habari ambazo hazikuwa nzuri kwa mashabiki wa Chameleone sasa ana onekana kuwa yuko vizuri na mkewe. Kwenye interview ya  Chameleone na Daniella waliyo ifanya na gazeti la The New Vision, wamesema kuwa hivi sasa wame tatua tofauti zao na mashitaka yaliyo kuwa yametolewa na Daniella tayali yamefutwa huko mahakamani..